Verse 1 (Mejja)
mpaka hapo mimi nipo
ukiniona niko simple
ni Majengo imenifanya mi kukaa nikiwa hivyo
yaani kwa ufupi ni Majengo imenilea
imenifunza kukaa na watu wako na umbea
imenifunza ku-budget ati nikiwa na soo
kuna blu ya dondo
blu ya mogoka
kuna blu ya njugu
blu ya kuchoma
ile blu imebaki beste yangu namwokoa
ndio sikuwangi selfish nadhani umelewa
akili ya biashara manze mi ndio ilinipea
utakaaje na njaa na unaishi na watu
si vizuri kuiba ni vizuri kupigana bafu
ndio ukiishi na mimi hauwezi lia njaa
mi ni superstar ku-hustle nikute kwa mtaa
asante Majengo kwa kunifungua akili
wee ndio umenijenga mpaka nikakuwa mimi
Chorus (Sheena)
oh Majengo asante
kwa yote uliyonipa
jijini zako ni fiti
ndio maana niko hapa
oh Majengo asante
kwa yote uliyonipa
jijini zako ni fiti
ndio maana niko hapa
Verse 2 (Mejja)
kushikwahshikwa Majengo na gava imesaidia
ile kuwachapa Kiswahili alafu wanakuwachilia
ndio mi hukuwa na lugha kupata manzi si shida
noma ni manzi akidai Mejja twende dinner
juu kutumia visu na umma itanishinda
Majengo ni ujanja Majengo ni kujitafutia
chunga usiwe tupu ukute umeandaliwa
siamini kusota ndio maskio sijalalia
nitafute kibarua ama nipite na zile chuma
niibe ile sufuria ama mkokoteni nitaskuma
ndio zetu vile anajua mwishowe nitakula
imenifunza ukiamua kitu, haurudi nyuma
ka pedi huuza ndukulu na haogopi kushikwa
juu asipouza hiyo siku hakutapikwa
asante Majengo kwa kunifungua akili
wee ndio umenijenga mpaka nikakuwa mimi
Chorus (Sheena)
oh Majengo asante
kwa yote uliyonipa
jijini zako ni fiti
ndio maana niko hapa
oh Majengo asante
kwa yote uliyonipa
jijini zako ni fiti
ndio maana niko hapa
Verse 3 (Mejja)
ukiniona nikiroga utaona aibu ilinitoka
juu nilikuwa hawker nikiuzia mashore ngotha
juu kazi ni kazi Majengo hakuna ufupa
ntakuuzia mudi mtura pia naeza choma
ilinifunza kupendana chokoza mtu wa Majengo
tunakuja sote unajua umechokoza moto
watoto, vijana na wazee hawana meno
na mama Wakiswahili wakiwa wamejifunga leso
na ukichokoza mtu wa Calif ni ka umenigusa
hata usijaribu kama hutaki kujuta
ila nikiwaza halafu niangalie nyuma
siskiangi aibu juu ya mahali nimetoka
Majengo imenijenga mpaka nimekuwa msanii
yale nimepitia ndio imeandika ngoma hii
asante Majengo kwa kunifungua akili
wee ndio umenijenga mpaka nikakuwa mimi
Chorus (Sheena)
oh Majengo asante
kwa yote uliyonipa
jijini zako ni fiti
ndio maana niko hapa
oh Majengo asante
kwa yote uliyonipa
jijini zako ni fiti
ndio maana niko hapa